HUDUMA ZA KIJAMII
Tanzania World Healing haitenganishi huduma ya kiroho na mahitaji ya kimwili ya jamii. Kupitia huduma za kijamii, kanisa linatekeleza upendo wa Kristo kwa vitendo. Baadhi ya huduma hizo ni:

Misaada kwa Wenye Uhitaji
Chakula, nguo na mahitaji mengine ya msingi hutolewa kwa watoto yatima, wajane, na familia masikini.

Uhifadhi wa Mazingira
Kainisa linajibidiisha katika kuhamasisha usafi na uhifadhi wa mazingira , kanisa hushirikiana na jamii kufanya usafi wa maeneo ya wazi na kutunza mazingira.

Huduma za Elimu
Kanisa hushiriki kusaidia watoto kutoka familia zisizojiweza kupata elimu kwa kutoa msaada wa karo na vifaa vya shule.

Afya ya Jamii
Huduma za afya kama kliniki za bure, vipimo vya afya, na elimu ya kinga dhidi ya magonjwa huendeshwa kwa kushirikiana na wataalamu wa afya.

