Huduma ya

Maombi na Ushauri

MAOMBI

Huduma za maombi ndizo msingi wa huduma ya World Healing. Kanisa linaamini katika nguvu ya maombi kama njia ya kuwasiliana na Mungu na kufungua milango ya uponyaji, ukombozi na mafanikio.

Maombi ya Kila Wiki

Kanisa huendesha ibada za maombi kila wiki zenye lengo la kujenga imani na kuimarisha maisha ya kiroho ya waumini.

Maombi ya Uponyaji

Waumini na watu wanaotafuta msaada wa kiroho hukaribishwa kupokea maombezi kwa ajili ya uponyaji wa magonjwa ya mwili, akili na roho.

Maombi ya Timu

Timu maalum ya waombezi hujitolea kuombea familia, jamii, taifa na makanisa mengine kwa ajili ya amani, mafanikio na uvuvio wa kiroho.

Maombi Maalumu

Kanisa huandaa makesha na makambi ya maombi mara kwa mara, ambapo waumini huombewa maono na mwelekeo wa maisha yao

USHAURI

Huduma ya Ushauri