UMISHENI NA UNAFUNZI

Umishenii na Uanafunzi ni moyo wa huduma ya Tanzania World Healing, ikiwa ni agizo kuu la Yesu Kristo kwa kanisa. Huduma hii inalenga kuwafikia watu walio mbali na neno la Mungu. Shughuli za umisheni ni pamoja na:

Shiriki nasi katika kueneza upendo wa Yesu Kristo

Uinjilisti wa Kijamii (Crusades)

Kanisa huandaa mikutano mikubwa ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya mijini na vijijini ili kuwafikia watu wengi kwa injili.

Upandaji wa Makanisa

Ili kuimarisha huduma ya neno katika maeneo mbalimbali, kanisa limeanzisha na linaendelea kuanzisha makanisa ya matawi sehemu tofauti za nchi.

Mafunzo kwa Wamishenari

Watumishi na waumini wenye wito wa umisheni hupewa mafunzo ya kiroho na kimkakati ili kuweza kufanya huduma kwa ufanisi katika mazingira tofauti.

Huduma kwa Makundi Maalum

Umisheni pia unalenga makundi ya watu kama wafungwa, wagonjwa hospitalini, watoto wa mitaani, na jamii zisizofikiwa kirahisi.

Ukurasa Huu Utawadia Hivi Punde