Ibada Zetu

KARIBU KWENYE IBADA ZA

World Healing Church

Tunapenda kukualika kwa moyo mkunjufu kwenye Ibada zetu za Jumapili, Jumatano na Ijumaa katika Kanisa la World Healing – kanisa lililojengwa juu ya msingi wa Injili safi ya Yesu Kristo, likiwa na kusudi la kubadilisha maisha kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu.

Ibada ya Jumapili

Muda wa Ibada              :

SAA 4:00 ASUBUHI

Tazama Mubashara        :

Tutembelee                    :

Sheli ya Kwalala,

Barabara ya Old Moshi 

Kijenge ya Chini, Arusha 

Ibada ya Jumapili ni Ibada ya furaha kuu kwa familia ya World Healing! Ni wakati wa kukusanyika kama mwili wa Kristo kumpa Mungu sifa, kuabudu kwa unyenyekevu na kupokea neno la uzima linalobadilisha maisha.

Ibada ya Jumapili inahusisha:

Sifa za nguvu na zenye upako:

Tunamwimbia Bwana kwa shangwe na furaha, tukimkiri kuwa mkuu juu ya yote.

Tunainua mioyo yetu mbele za Mungu kwa nyimbo za ibada zinazoleta uwepo wa Mungu wa kipekee.

Mchungaji na watumishi waliopakwa mafuta huleta ujumbe wenye kuelekeza, kufariji, na kutia nguvu kwa maisha ya kila siku.

Baada ya neno, kuna nafasi ya kupokea maombi kwa ajili ya uponyaji, ukombozi, na msaada wa kiroho.

Ibada ya Jumatano

Ibada ya Jumatano ni ya wanafunzi wa kweli wa Kristo – wale wanaotamani kulielewa Neno kwa undani na kulionyesha katika maisha ya kila siku.

Katika ibada hii:

Muda wa Ibada              :

SAA 11:00 JIONI

Tutembelee                    :

Sheli ya Kwalala,

Barabara ya Old Moshi 

Kijenge ya Chini, Arusha 

Ibada ya Ijumaa

Ijumaa ni siku ya  vita vya kiroho na kuvunja minyororo ya giza! Huduma hii ni maalum kwa maombi ya nguvu, maombezi, na ukombozi kwa kila eneo la maisha.

Unapohudhuria:

Muda wa Ibada              :

SAA 11:00 JIONI

Tutembelee                    :

Sheli ya Kwalala,

Barabara ya Old Moshi 

Kijenge ya Chini, Arusha 

Usikose nafasi ya kuonja uwepo wa Mungu, kusikia sauti Yake, na kuanza safari mpya ya kiroho yenye uzima wa milele. Hakika utasema, “Hakuna kama Bwana wetu!”

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi: Simu: +255 123 456 789 | Barua pepe: katibu@worldhealingtv.org