Ibada ya Jumapili Hii

SAA 4:00 Asubuhi - SAA 7:00 Mchana

Jiunge Nasi Mubashara

KARIBU

World Healing Church

“Imani Inaachia Nguvu”

Kanisa la World Healing ni huduma ya Kikristo iliyojikita katika urithi wa kiroho Afrika. Tumejitolea kutangaza Injili ya Yesu Kristo, kubadilisha maisha, na kuinua ustawi wa jamii za Kiafrika na kwingineko kupitia nguvu za Roho Mtakatifu. Kwa njia ya ibada na uinjilisti, uanafunzi, na huduma za kiutu, tunatangaza upendo wa Mungu kwa watu wa asili zote.

Dhamira yetu ni kuhubiri Injili, kufanya wanafunzi, na kuhudumia jamii zenye uhitaji kupitia nguvu ya Injili ili kuwa na ulimwengu uliyobadilishwa ambapo kila mtu anapata upendo wa Kristo na anaishi kwa matumaini, heshima, na kusudi la Mungu.

HUDUMA ZETU

Maombi

Maombi ndiyo msingi wa Kanisa la Word Healing. Tunaamini katika nguvu ya maombi kuwa ni njia ya kuwasiliana na Mungu na kufungua milango ya uponyaji na ukombozi.

Umisheni

Umisheni ni moyo wa huduma ya Kanisa la World Healing, ikiwa ni agizo kuu la Yesu Kristo kwa kanisa lake. Huduma hii mi kwa ajili ya kuwafikia walio mbali na neno la Mungu

Jamii

World Healing Church haitenganishi huduma ya kiroho na mahitaji ya kimwili ya jamii. Kupitia huduma za kijamii, kanisa linatekeleza upendo wa Kristo kwa watu wote.

IBADA ZETU

Msingi wa huduma yetu ni ibada zinazoongozwa na Roho Mtakatifu, zinazobadilisha maisha, maombi yenye nguvu, na mafundisho yenye matokeo yanayojikita katika Neno la Mungu.

Tunakualika kwa moyo mkunjufu kwenye Ibada zetu JUMAPILI | JUMATANO | IJUMAA

Ibada ya Jumapili

SAA 4:00 ASUBUHI

Ibada ya kumpa Mungu sifa, kuabudu kwa unyenyekevu na kupokea neno la uzima linalobadilisha maisha.

Taarifa Zaidi

Ibada za Jumatano

SAA 10:00 JIONI

 Ikiwa unatamani kulielewa Neno kwa undani na kulionyesha katika maisha ya kila siku, karibu kwenye Ibada hii.

Taarifa Zaidi

Ibada za Ijumaa

SAA 10:00 JIONI

Ibada ya vita vya kiroho na kuvunja minyororo ya giza, maombi, maombezi, na ukombozi kwa kila eneo la maisha.

Taarifa Zaidi

HABARI NA MATUKIO